September 28, 2014


SAMATTA

Wakati AS Vita imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, deni linakwenda kwa Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Wawili hao wana kazi ngumu ya kuivusha TP Mazembe hadi fainali wakati itakapokutana leo na Entente Setif ya Algeria.

Setif ilishinda kwa mabao 2-1 katika mechi yao ya kwanza ikiwa nyumbani. Wakati mechi hiyo ya mjini Lubumbashi, DR Congo inasubiriwa kwa hamu kubwa.
Hata hivyo Mazembe inajivunia rekodi yake nzuri ya kushinda mechi tano, ikifunga mabao tisa na kufungwa moja tu.
Kutokana hali hiyo, Samatta ndiye amekuwa kiongozi wa mashambulizi wa Mazembe.
Leo atakuwa na kazi ngumu na iwapo Ulimwengu naye atapata nafasi hiyo, basi ataungana kwenye presha hiyo ya kuingia fainali.
Presha itakuwa kubwa kwa kuwa wapinzani wao AS Vita wametinga fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic