Kocha Mkuu wa Coastal
Union, Yusuf Chippo ameendelea kulia kwamba ‘wamenyongwa’ mjini Mbeya.
Chippo raia wa Kenya amesema walifanya kila linalowezekana, lakini
mwisho wakapewa penalti ya mizengwe.
“Unajua kama tungekuwa tumefungwa tu, sina sababu ya kulalamika
kwa kuwa ndiyo mpira wenyewe.
“Ambacho ningefanya ni kujipanga na kuangalia mechi inayofuata. Lakini
tulichofanyiwa si kitu kizuri.
“Wenyeji waliona mambo hayakuwa mazuri na huenda wasingepata
penalti ile na kutangulia, basi tungewaangusha, si kitu kizuri kuwa na matokeo
ya kuipendelea timu fulani,” alisema Chippo.
Coastal Union imefungwa mechi hiyo kwa bao 1-0 ikiwa ni mechi yake
ya pili baada ya kuanza kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Polisi Moro.
0 COMMENTS:
Post a Comment