Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema anashangazwa na Yanga kuanza
kulaumu kuwa Simba imefanya ujanja wa mechi yao ya Oktoba 12 kusogezwa mbele.
Hans Poppe amesema Simba
haina sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa Yanga ni wepesi, hata kama Simba
ingeshituliwa usingizini ili kucheza nao, ni lahisi tu kuwamaliza.
Baada ya TFF kuusogeza
mbele mchezo wa watani, baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wamekuwa
wakilalamika kwamba Simba imefanya ‘mipango’ ili mchezo usogezwe ikihofia kuwa
na majeruhi wengi.
“Kama kipa tunao watatu,
Ivo si kipa pekee Simba. Yuko Casillas na Manyima na wote ni makipa wazuri.
“Ukizungumzia mabeki wako
wengi unawaona, Mgeveke na wengine wapo na wanacheza vizuri tu.
“Kama ni Kiongera, Simba
ina washambuliaji wengi sana. Wananishangaza sana hawa watu, Yanga ni wepesi na
Simba ipo tayari kupambana nao wakati woeote na kuwashinda.
“Hata ikiwa ni usiku,
wakatushtua, tuna uwezo wa kucheza nao na kuwashinda,” alisema Hans Poppe
akihojiwa jijini Dar.
TFF imesema itatangaza
kesho kuhusiana na mchezo huo utachezwa ligi baada ya leo kutangaza kuusogeza
mbele kutokana na kuitumia tarehe hiyo kwa mchezo wa kirafiki wa kimataiga na Taifa Stars itaivaa Benin.
0 COMMENTS:
Post a Comment