DK NDUMBARO (KUSHOTO) WAKATI AKIWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA. |
Klabu 14 za Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa zitamtumia mwanasheria
maarufu nchini, Dk Damas Daniel Ndumbaro kuwatetea kuhusiana na suala la TFF
kukata fedha zao kutoka kwa wadhamini.
TFF imekaa na kujadili, halafu ikakubaliana kuwa fedha za
wadhamini kutoka Azam TV na Vodacom, asilia tano zikatwe kutoka kwa kila
mdhamini, halafu ziingie TFF kusaidia soka.
Jambo hilo la kwanza la kushangaza katika mchezo wa soka nchini na
duniani kote, liliandikwa kwa mara ya kwanza na SALEHJEMBE.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Dk Ndumbaro amethibitisha hilo amesema
tayari klabu zimeweka wazi kuhusiana na msimamo wao.
“Klabu zote 14 zinapinga kwa nguvu uamuzi huo wa TFF kutaka
kuzikata fedha zao za udhamini wa Azam TV na Vodacom.
“Kuhusiana na mgawo, kila kiko wazi kwamba kila upande unapata
kiasi gani.
“Kwa pamoja klabu zina ushauri, kwamba kama kuna fedha
inahitajika, basi TFF inaweza kuchukua mgawo wake na kuutumia na si fedha za
klabu ambazo zina majukumu mengi ikiwemo kuweka kambi, mishahara na uendeshaji
wa timu ili ligi iendelee,” alisema Dk Ndumbaro.
Uamuzi huo wa TFF umeonyesha kuwashangaza wadau wengi hasa
kuhusiana na kutaka kuchukua hadi fedha za wadhamini wa klabu. Bodi ya Ligi
Tanzania, bado haijatoa uamuzi wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment