September 30, 2014

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR.
Suala la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka lipewe asilimia tano kutoka kwenye udhamini wa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, linazidi kuchukua sura mpya.

Klabu mbili za Mtibwa Sugar na Mbeya City zimetishia kufungua kesi kwa Bodi ya Ligi Tanzania au watendaji wake iwapo itakubaliana na suala hilo la kutoa fedha zao za udhamini kwa TFF.
Mwanasheria wa klabu zote 14 ambaye anawatetea katika suala hilo, Dk Damas Ndumbaro amesema Mtibwa na Mbeya City wamefikia uamuzi huo.

"Ni kweli Mbeya City na Mtibwa wamefikia uamuzi huo na bodi wanalijua hilo.
"Wanaona ni kama kuwaonea na kila kitu kiko wazi kuhusiana na mgawo. Wamesema iwapo bodi itakubaliana na TFF, basi mara moja wao watafungua kesi," alisema Dk Ndumbaro.
Tayari klabu hizo 14 kwa pamoja zimetoa tamko la kupinga kwa nguvu zote suala hilo jipya na la aina yake katika soka nchini kutoka kwa TFF.
TFF inataka ipewe asilimia 5 kutoka kwenye fedha za udhamini klabu inazopata kutoka Vodacom na Azam TV!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic