Difenda, Mamadou Sakho amewaomba
radhi mashabiki wa Liverpool kutokana na kitendo chake cha kuondoka Anfield
dakika chache kabla ya mechi dhidi ya Everton.
Sakho aliondoka baada ya
kocha wake Brendan Rodgers' kuamua kumtumia Martin Skrtel badala yake.
Kutokana na hali hiyo,
difenda huyo mwenye umri wa miaka 24, aliamua kuondoka zake kwa hasira.
Kutokana na hali, baadaye
alitumia mtandao wa kijamii na kusema anaamini haukuwa uamuzi sahihi.
“Nilijisikia vibaya na
kuona haukuwa uamuzi sahihi mimi kuondoka wakati ule.
“Naomba mniwie radhi kwa
kitendo hicho ambacho hakikuwa cha kiungwana,” aliandika.
0 COMMENTS:
Post a Comment