TP Mazembe imefanikiwa kuishinda ES Setif ya Algeria kwa mabao 3-2 katika mechi iliyomalizika hivi punde mjini Lubumbashi.
Lakini ushindi huo umeshindwa kutosha kwa kuwa Mazembe wanayoichezea Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu haitakwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi ya kwanza Setif ilishinda kwa mabao 2-1, hivyo kufungwa 3-2, maana yake jumla ya mabao 4-4 lakini Setif inapata nafasi ya kwenda fainali kutokana na idadi ya mabao mawili ya ugenini.
Katika mechi ya leo, Mazembe ambayo iliwatumia Samatta na baadaye Ulimwengu ilifanya juhudi kubwa kushinda, lakini mabao mawili yakawatibulia.
Daniel Niii, Salif Coulibaly na Jonathan Bolingi ndiyo waliifungia Mazembe mabao matatu huku Abdemalek Ziaya na Soufiane Younos wakifunga mabao ya Setif.
Sasa Setif inakutana na timu nyingi ya DR Congo. Vita Club ambayo imeingia fainali baada ya kuwatoa Watunisia.
0 COMMENTS:
Post a Comment