Kocha wa Manchester United,
Louis van Gaal sasa ana kikosi kipana na anaweza kubadili hadi wachezaji wanane
nab ado akacheza akiwa hana hofu.
Tokea alipopata sare na
Sunderland ikiwa ni mechi yake ya pili ya Ligi Kuu England, van Gaal ametumia
pauni milioni 96 kwa ajili ya usajili.
Kutokana na sasa kuwa na
kikosi kipana kama kile cha Chelsea au Manchester City, van Gaal anaweza
kubadili wachezaji au vikosi tofauti anavyotaka yeye.
Angalia namna Mholanzi huyo
atakavyokuwa ‘komfotabo’ na vikosi hivi viwili na bado anaweza kubadili tena.
0 COMMENTS:
Post a Comment