Mshambuliaji Robin van
Persie amesema anataka kuichezea Uholanzi katika michuano ya Kombe la Dunia
itakayofanyika nchini Russia mwaka 2018.
Wakati huo van Persie
atakuwa na miaka 35, lakini amesisitiza anataka kuendelea kucheza hadi
atakapofikisha miaka 40.
Van Persie ambaye sasa ana
miaka 31, anaamini atacheza soka hadi akiwa na miaka 40.
Mholanzi huyo alikuwa kati
ya wachezaji waliofanya vizuri kwenye Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil,
akifunga moja ya bao bora la michuano hiyo na jingine lililoisaidia Uholanzi
kushika nafasi ya tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment