Mwamuzi
wa daraja la kwanza (class one), Luteni Godwill David Lugenge aliyefariki dunia
juzi (Septemba 7 mwaka huu) kwa ajali ya gari katika Wilaya ya Handeni mkoani
Tanga anaagwa leo (Septemba 9 mwaka huu).
Mwili
wa marehemu ambao umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo,
baadaye leo saa 6 mchana utapelekwa nyumbani kwa kaka yake Kimara Bucha jijini
Dar es Salaam ambapo shughuli za kuaga zitafanyika kabla ya safari ya kwenda
mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.
Luteni
Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani ya utimamu wa mwili kwa
waamuzi wa Ligi Kuu, akiwa na ndugu yake Christopher Alexander Lunyungu katika
gari dogo walipata ajali hiyo wakati wakienda mkoani Kilimanjaro.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambalo limetoa ubani wa sh. 200,000 kwa
familia ya marehemu kwenye shughuli ya kuaga itawakilishwa na mjumbe wake wa
Kamati ya Utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Saloum Umande
Chama.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi wa Mpira
wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana
ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe
0 COMMENTS:
Post a Comment