Na Saleh Ally
VIGUMU kuamini kama Kocha Arsene Wenger amekitengeneza kikosi chake
katika ubora wa juu na kinaweza kuwa ni kati ya vikosi vyenye nafasi kubwa ya
kutwaa ubingwa wa England.
Inakuwa ni vigumu kwa wengi kuamini kweli kikosi cha Arsenal
kinaweza kubeba ubingwa kwa kuwa kimekuwa kikianza vema na mwishoni kuishia
kugombea nafasi ya nne au tatu.
Hata hivyo, kitendo cha kutwaa ubingwa wa Kombe la FA msimu uliopita
kinaonyesha imani ya mashabiki wake inaweza kupanda na hadi ligi imechezwa
mechi 120, yaani kila timu mechi sita, Arsenal inaonekana iko kwenye takwimu za
juu katika timu zinazomiliki mpira vema.
Inawezekana timu ikamiliki mpira sana lakini isifanye vizuri, lakini
kiufundi hata aina mpya bora ya ulinzi ni timu kumiliki mpira mwingi kwa kuwa
ukiwa nao, hakuna anayeweza kukupokonya.
Ukiachana na umiliki wa mpira, Arsenal ndiyo timu inayoongoza kwa
kuwa na pasi nyingi zaidi zilizofika katika mechi hizo 120 za Premier League
zilizopigwa msimu huu.
Ina asilimia 87.2 ambayo ni ya juu zaidi na hii ni silaha nyingine,
kwamba timu inayofikisha pasi nyingi sehemu sahihi inakuwa na nafasi nzuri ya
kufanya vizuri kwa kuwa inatekeleza kilicho sahihi katika mipango yake.
Kama timu itakuwa inapoteza pasi nyingi, maana yake inajiondoa
kwenye reli au inajitoa kwenye mipango sahihi inayolenga kufanya.
Unaweza kusema ni kawaida Arsenal kumiliki mpira sana na kupiga pasi
za uhakika zaidi, lakini katika mechi hizo 120, Arsenal iko kwenye moja ya timu
zinazocheza soka la kibabe.
Arsenal inashika nafasi ya pili kwa timu ‘zinazochafua’ mchezo,
kwani tayari vijana hao wa Arsenal Wenger wana kadi 16 katika mechi sita.
Wanaoongoza ni Man City wakiwa na 17, utaona tofauti ilivyo ndogo.
Kinachovutia zaidi, Arsenal ina mchezaji katika listi ya wachezaji
wababe ndani ya mechi 120. Calum Chambers ndiye anaongoza kundi la wachezaji
wenye kadi nyingi, ana nne.
Hii inaonyesha sasa kuna mabadiliko makubwa kwa Arsenal, kwamba wana
uwezo wa kucheza mechi kwa aina zote. Pasi na urembo mwingi lakini
ikishindikana basi ‘wanakichafua’ na kucheza kibabe.
Mashabiki wa Arsenal wa Tanzania wamekuwa na hofu kama wengine
duniani, wanaiamini timu yao, tatizo ni inavyomaliza. Kwa mabadiliko haya ya
mapema, kunaweza kuwa kitu kipya, endelea kufuatilia.
UMILIKI WA MPIRA:
Arsenal
63.9%
Man Utd 60.3%
Everton
59%
Man City
58.9%
Newcastle
56.2%
PASI ZILIZOFIKA:
Arsenal
87.2%
Man City
86.6%
Man Utd
86.5%
Chelsea
85.5%
Everton
85.1%
PASI ZA MABAO:
Cesc Fàbregas Chelsea 6
Gylfi Sigurdsson Swansea 4
Stephen Quinn Hull 3
Jason Puncheon Crystal
Palace 3
Stewart Downing West Ham 3
VIKOS VIBABE:
Man City
17
Arsenal 16
West Ham 14
Swansea 11
Hull 12
WACHEZAJI WABABE:
Calum Chambers
Arsenal 4
Jason Puncheon Crystal Palace 2
Tyler Blackett Man Utd 2
Wayne Rooney Man
Utd 2
0 COMMENTS:
Post a Comment