PLUIJM |
Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Soka la Ghana (GFA) limeiagiza klabu ya Berekum Chelsea kumlipa kocha wake wa zamani, Hans van
der Pluijm ambaye aliwahi kuinoa Yanga kitita cha dola 215,000 (zaidi ya Sh
milioni 361).
Chelsea hiyo ya Ghana ilifanya vziuri kwenye Ligi ya mabingwa Afrika
ikiwa na kocha huyo, lakini baadaye wakafikiana kuvunja mkataba.
Lilipofikia suala la malipo, Chelsea wakawa wagumu na kusababisha Pluijm
kufungua kesi kwenye shirikisho hilo.
Tayari shirikisho hilo limehibitisha kuidhinisha malipo hayo kwa Pluijm
ambaye aliiongoza Yanga kuilaza Al Ahly jijini Dar es Salaam, lakini Yanga
ikang’olewa kwa mikwaju ya penalti.
Akizungumza jana na Championi Jumatano kutoka Accra, Ghana, Pluijm
alisema kweli hilo limepitishwa na shirikisho hilo, lakini Chelsea wamekataa.
“Wana nafasi ya kukata rufaa, lakini wameishasema ni kiasi kikubwa. Hivyo
ninasubiri kwanza, sasa sitaweza kulizungumzia kwa undani,” alisema.
Baada ya hapo, Pluijm aliamua kuodoka kwenda Saudi Arabia akimtwaa na
Charles Boniface Mkwasa kwenda kumsaidia kazi katika klabu ya Al Shaollah ya
nchini humo.
Hata hivyo, walishindwana na Mholanzi huyo akarejea Ghana ambako ameoa
raia wa nchini hiyo na Mkwasa amerudi nyumbani ambako ameula sasa ameajiriwa na
TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment