October 18, 2014

MANYIKA (KATIKATI) AKIPATA MAFUNZO NCHINI AFRIKA KUSINI.

Kipa kinda Peter Manyika ambaye amecheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara, halafu ikiwa ni dhidi ya watani Yanga, amesema baba yake ndiye silaha yake kubwa.


Peter ni mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Manyika Peter na leo alikuwa langoni wakati Simba ikitoka sare ya bila kufunga na Yanga.
Manyika ni kipa wa tatu wa Simba, lakini alilazimika kukaa langoni kutokana na kipa namba moja, Ivo Mapunda kuwa majeruhi, hali kadhalika Hussein Shariff ‘Casillas’ pia ni majeruhi.
“Baba ndiye amekuwa silaha yangu, ananishauri na kunieleza nini cha kufanya.
“Lakini nawashukuru wenzangu, wamekuwa wakinipa maoni, wamenishauri mambo mengi na pia kunipa moyo leo kuwa ninaweza,” alisema Manyika.

Kipa huyo amedaka katika mechi hiyo kubwa huku akionyesha utulivu wa hali ya juu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic