October 1, 2020

 


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa ulikuwa ni mpango maalumu kumuingiza nyota wao Wazir Junior kipindi cha pili na kumtoa baada ya kuyeyusha dakika 15 uwanjani.


Jana Septemba 30, Uwanja wa Azam Complex wakati Yanga ikishinda kwa mabao 2-0 mbele ya KMKM kwenye mchezo wa kirafiki, Junior aliingia kipindi cha pili na alitumia dakika 15 uwanjani kisha akatolewa nafasi yake ikachukuliwa na Farid Mussa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa Wazir ni mchezaji wa Yanga na alipewa majukumu maalumu ndani ya dakika ambazo alizitumia ndio maana alipokamilisha kazi yake alitolewa.

"Alipewa kazi maalumu ya kufanya na benchi lilipoona ameweza kutimiza majukumu hayo kwa muda aliopewa alitolewa nje na jukumu lake akapewa mchezaji mwingine.

"Kwa wakati huu bado tupo kwenye kutengeneza timu na ukizingatia mechi ni ya kirafiki hakuna tatizo lolote kila mchezaji ana nafasi yake ndani ya timu na majukumu ni tofauti kabisa, mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti," amesema.


Junior ni ingizo jipya ndani ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ambapo aliibukia ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Mbao FC ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.


Msimu wa 2019/20 ndani ya ligi alitupia jumla ya mabao 12 na kuwa miongoni mwa wazawa wenye mabao mengi nyuma ya Meddie Kagere wa Simba ambaye alitupia jumla ya mabao 22. 

Msimu huu bado hajaanza kuonyesha makeke yake ndani ya Yanga kwenye ligi kwa kuwa bado hajapewa majukumu kwenye mechi za ligi kutokana na uwepo wa Michael Sarpong ambaye ndiye mshambuliaji namba moja wa Yanga kwa sasa.


Sarpong kwenye mechi nne za ligi ametupia bao moja kibindoni ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.

5 COMMENTS:

  1. Ujinga mtpu kazi gani maalum kwenye mechi ya kirafiki? Yanga na benchi lao la ufundi wamechangikiwa.
    Tulizungumza mapema kwamba kama Yanga wanataka kujichanganya mapema kwenye ligi na hata kwenye mipango yao ya kuijenga Yanga ya kiushindani basi watake kujilinganisha na wanachokipata simba kwenye mechi zao yaani yanga kulazimisha kupata matokeo ya ndani ya uwanja na nje ya uwanja kama simba kwa hivi sasa. Yanga wanaweza wakabahatika wakamfunga simba. Wanaweza pia wakajaza uwanja wa mkapa na simba wakashindwa kujaza.Yanga hao hao wanaweza kumsaini mchezaji amabe anatakiwa na simba. Yanga hao wanaweza kuwa na mapokezi mazuri ya wachezaji wao wapya kuliko simba ila ukweli utabakia pale pale kuwa hakuna njia ya makato katika kupata mafaniko ya kweli. Simba hawa hawa walishajaribu mambo mengi ya ubabaishaji kutaka kupata mafanikio ya kweli ila hawakuwahi kupata kile hasa wanachokipata mpaka walipoamua kujikusanya na kuamua kwanza kuunda taasisi imara ya kusimamia timu ili kuunda timu imara.Na sasa kwa kiasi kikubwa ukiiangalia simba unaona kabisa kuwa wanashabaha ya kweli ya kutafuta mafaniko ya kweli ya timu yao na wakiendelea hivi walivyo sasa basi hayo yajayo yanayotarajiwa kuwafurahisha wanasimba hayapo mbali.Timu ile ya simba tunayoiona ikicheza pale kwa mkapa ikitoa burudani nzuri haikujengwa kwenye msimu huu wa usajili yaani simba kama ni dishi la kupikia ubwabwa basi ni dishi lililokwisha komaa masizi hata likipata moto vipi si rahisi kuunguza ubwabwa. Ukiiangalia timu ya yanga bado ni sawa na sufuria jipya wawe na subira ili likomae kuja kuwapikia chakula kizuri la sivyo papara zao watakula chakula wasichokipenda kila siku. Waipe timu muda wasilazimishe timu yao kutaka kucheza kama inavyocheza simba kwa mapema mno wa msimu ligi wataharabikuwa.

    ReplyDelete
  2. Mawazo mazuri lkn kila Timu itacheza brand ya mpira wa Simba,au Timu kuwa nzuri unaipimaje ,
    Kwani Simba imefanikiwa Kwenye lipi hasa Uwanjani?Kipimo Ni kufunga Ihefu ambaya Budget yake yote ni Gharama ya Usajili wa Morrisoni,unataka utuaminishe Ni uwekezaji gani nje ya Azam,Simba ,Yanga hizi Timu mnazofunga na kujinadi mnajua Zina budget gani zaidi ya kuokoteza Wachezaji na vilevile mkipambana kwa nguvu nje ya Uwanja kusaidiwa na marefa wanaoshindwa kutafsiri sheria kwa makusudi au bahati mbaya wanatoa fever kwenu unnecessarily ,hizo mechi tunaziangalia wote
    Sasa je Kama issue ni Wachezaji Wageni Yanga na Kipimo ni Simba,mbona hizo Timu zote mmefunga hata hao Gwambina Wana wachezaji wapya na Wana field zaidi ya 7 au 8 wapya angalia mechi ya Simba na Gwambina wengi wapya,Mtibwa the same ,Ihefu 5 wapya nk ,na mkiwafunga mnahisi ninyi Ni bora .Maana yangu siyo kila kitu tuoneshe Simba Kama mfano ,kwani Waliyo nayo Azam(Uwekezaji)Simba hata nusu wanafika? na Kama kigezo ni ku dominate ligi kwa kipindi fulani kwani kwa Simba hii ni mala ya kwanza?Kifupi tuache tabia ya mahaba na Fitna zituongoze .Kocha kasema mcheZaji alifanya hivi wewe unaanza hisia zako .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu, una mashaka na ubora wa Simba ukilinganisha na Yanga? Mimi mwenyewe Yanga lakini nakubali kwamba Simba ni bora zaidi yetu. Utake usitake, Simba ni taasisi inayojiendesha kwa weledi na ndio maana inapata mafanikio. Tangu waingie kwenye mfumo mpya wa kuendesha klabu mafanikio yao yameonekana dhahiri: Wametwaa ubingwa wa VPL mara tatu mfululilo, pia wametwaa Ngao ya Hisani mfululilo na wamefika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Unataka mafanikio gani zaidi ya hayo? Sisi Yanga ni lazima tujipange na kufuata nyayo za Simba ili tupate mafanikio. Si sahihi kuibeza Simba na kudhani hatuna cha kuiga. Tusijidanganye!

      Delete
  3. Hiyo burudani unaipima against which opponent Kati ya hao uliyocheza nao ,Timu zinawekeza Uingereza eg Chelsea ,Man City ,Man U na zote za Ligi za Ulaya na tunaona bt hii Ligi yetu njaaa tupu eti burudani kwa Mkapa kwa mpira upii na marefa always advantages on your side,creating pressure on opponent once results are not on your fever muone aibu.

    ReplyDelete
  4. Vile vile ninyi Waandishi wa mpira mmekuwa sehemu ya kuleta mtafaruku Yanga,leo TBc wanahoji watu was mtaani wanokosoa uwezo wa Kocha Yanga ,halafu mwisho anahojiwa Habib Kondo wa KMC .Je Kama ni taarifa si wamhoji msemaji wa Yanga? Hizo fununu zikitokea Simba utasikia Haji Manara kila Redio kwa Yanga una hoji layman mwingine yupo kwenye bucha kavaaa ma uniform .Bt tunajua matokeo ya Yanga yamewastua mnajaribu ku destabilize Yanga bt hatuwasikilizi.Mlisema Viwanja vigumu Leo wamepasua eti goli moja Tena anafunga beki .Kwa mnaojifanya kuendelea hizo habari zinatija?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic