SHABIKI MBEYA CITY, AKIONYESHA ALIVYOJERUHIWA. |
Uongozi wa Mbeya City umetoa
tamko la kulaani kupigwa kwa mashabiki wao kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi
ya Ruvu Shooting iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, jana.
Mechi hiyo ilimalizika kwa
suluhu na kuwa sare ya pili ya Mbeya City dhidi ya timu za jeshi. Mechi ya
kwanza mjini Mbeya iliyoka sare na JKT Ruvu.
Uongozi huo kupitia Ofisa Habari
wake, Dismas Ten umesema kuwa sehemu hiyo si salama. Soma tamko lao.
“Inasikitisha sana, wanajeshi
jana walianza kuwapiga mashabiki wa Mbeya City FC, kwa sababu
walikuwa wakizunguka uwanjani kushangilia.
“Tatizo lilianza pale
walipokwenda kwenye lango la Mbeya City na kipa wetu David Buruhani muda
wote alikuwa akibughuziwa na kundi la watu wanaoaminika ni askari lakini
walikuwa wamevaa kiraia.
“Ghafla Wanajeshi wakaja juu na
kuanza kuwapiga mashabiki wetu, Uwanja wa Jeshi timu ya Jeshi, kuna haja TFF
kuangalia hili.
“Raia wananyanyasika! Uwanja wa Mabatini
siyo sehemu salama kwa raia hasa timu yao inapokuwa na matokeo mabovu, uwanjani
kunakuwa hakuna ruhsa ya kushangilia timu pinzani.”
0 COMMENTS:
Post a Comment