October 5, 2014


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aneonekana kushitukia mchezo kwamba huenda mshambuliaji diego Costa hana tatizo kuwa sana kwenye myama zake za paja huku akisema Mhispania huyo anaamini yeye ni muuaji.

Wenger ametaka suala hilo kutokuwa ndiyo hoja ya kujadiliwa na kusema anavyocheza Costa, haonyeshi tena kama ana tatizo hilo.

“Tumejiandaa vizuri kupamabana naye pamoja na kikosi cha Chelsea. Costa ni mshambuliaji hatari ambaye kocha yoyote angeweza kutamani kuwa naye kwa kuwa anajisikia yeye ni muuaji.
“Anapokuwa mbele ya lango, kweli Costa ni muuaji, hataki utani na ndiyo maana ana mabao nane hadi sasa, si jambo dogo.
“Tuliona ana tatizo hilo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Atletico, lakini kwa sasa naweza kusema yuko vizuri tu, nasi tuko tayari,” alisema Wenger akionyesha kujiamini.

Chelsea inakutana na Arsenal kwenye Ligi Kuu England leo, zote zinatokea London lakini Arsenal watakuwa darajani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic