Toto African na Friends Rangers wameendeleza ushindi kwenye Ligi
Daraja la kwanza baada ya kushinda mechi zao za pili mfululizo.
Toto African imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Burkina Fasso ya
Morogoro.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Toto
ilitoka nyuma kwa bao moja na kusawazisha kabla ya kupata la ushindi.
Nayo Friends imeshinda kwa bao 1-0 lililopatikana kwa mkwaju wa
penalti dhidi ya African Lyon.
0 COMMENTS:
Post a Comment