Kocha Arsene Wenger amesema
wala hatajuta kutokana na kitendo chake cha kumsukuma Kocha wa Chelsea, Jose
Mourinho.
Wenger alishikana na
Mourinho wakati timu zao zilipokutana kwenye mechi ye Premier League kwenye
Uwanja wa Stamford Bridge na Arsenal ikalala kwa mabao 2-0.
“Nini cha kujuta, wala
sitafanya hivyo. Nilikuwa ninatoka upande mmoja kwenda mwingine.
“Nilipogeuka nikakuta mtu
yuko mbele yangu kabisa kanizuia.
“Halafu hasemi lolote, sasa
unafikiri nitafanya nini,” alisema Wenger.
Mwamuzi wa akiba
alilazimika kuingia kati kuwatenganisha makocha hao wasifikie kuchapana
makonde.
Baadaye mwamuzi wa mchezo
naye aliwaita na kutoa onyo kali akitishia kuwatoa uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment