Wakati
fulani, aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho aliwahi kutoa kauli hii: “Kama
hauna mbwa, basi unalazimika kuwinda hata na paka.”
Ilionekana
ni kama dharau kwa mshambuliaji Karim Benzema, akinaanisha hana sifa za kuwa
namba tisa sahihi.
Kauli
hiyo ya Mourinho imekuwa ikizua mijadala ya kila aina kuhusiana na ubora wa
Benzema.
Lakini
takwimu sasa zinamlinda na kuonyesha Benzema ni bora hata kuliko Gonzalo Higuaín.
Benzema alifunga mabao 26 baada ya kucheza mechi 57 za msimu uliopita lakini
akafanya vizuri zaidi katika mechi zenye presha kubwa dhidi ya Barcelona.
Kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo usiseme, takwimu zinaonyesha Benzema amefunga
mabao 38 katika mechi 67 alizocheza.
Mabao
yanamfanya awe na wastani wa 0.57 ya bao kwa kila mechi.
Ajabu
wako hadi sasa wanahoji uwezo wake, wakati wanamuita mshambuliaji mpya wa
Atletico Madrid ambaye alikuwa Bayern Munich Mario Mandzukic, kuwa ni aina ya mfungaji bora kwa upande wa
washambuliaji.
Mandzukic
yeye amefunga mabao 18 katika mechi 53 za Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumpa
wastani wa 0.34 ya bao kwa mechi ambayo ni chini ukilinganisha na ile ya
Benzema.
Hii
inaonyesha kiasi gani wako wale ambao wamekuwa hawampendi tu Benzema au ana
bahati mbaya kwani kwa takwimu, zinaonyesha ni mmoja wa washambuliaji bora
kabisa duniani.
0 COMMENTS:
Post a Comment