| MWADUI |
Kikosi cha Toto African ya Mwanza, kimeichapa FC
Panone katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Toto African inayofundishwa na John Tegete, baba
mzazi wa mshambuliaji Jerry Tegete wa Yanga, imeibuka baada ya kupoteza mechi
iliyopita lakini iko kwenye listi ya timu zilizoshinda mechi tatu.
Wakati Toto inashinda, Mwadui FC inayofundishwa
na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imeichaoa Rhino Rangers ya Tabora kwao kwenye Uwanja
wa Ali Hassan Mwinyi.
Kikosi hicho cha Julio kilipata mabao yake kila
kipindi na kujiweka vizuri kwenye vita ya kurejea Ligi Kuu Bara.
Ashanti nayo ilichezea kipigo kutoka kwa Tesema
wakati Lipuli nayo iliibuka kwa kupata ushindi baada ya kuwa ikiambulia sare na
vipigo.







0 COMMENTS:
Post a Comment