Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga
ameamua kuacha kazi katika taasisi hiyo muhimu katika mchezo wa soka nchini.
Taarifa zinaeleza Mwakibinga amejiweka pembeni
ni kutokana na mvutano huo uliopo baina ya pande mbili, kati ya TFF na klabu
zinazopinga makato hayo.
Mvutano huo ulizuka hivi karibuni baada ya Rais
wa TFF, Jamal Malinzi kutoa agizo la timu zote kukatwa asilimia tano za
wadhamini, jambo ambalo lilikataliwa na klabu na kuamua kumteua mwanasheria,
Damas Ndumbaro kusimamia haki yao.
Mwakibinga amesema kwa kifupi kuwa, ameamua
kuachia ngazi tangu juzi Oktoba 31, bila kuweka bayana sababu za kuachia ngazi.
“Nipo kwenye kelele lakini napenda kukwambia
kwa kifupi kuwa nimeacha kazi ya kuiongoza Bodi ya Ligi,” alisema Mwakibinga.
Alipoulizwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine
Mwesigwa, alithibitisha juu ya kuacha kazi kwa Mwakibinga, licha ya kusema kuwa
bado hawajapokea barua rasmi kutoka kwake.
“Nimesikia juu ya kuacha kazi kwa Mwakibinga,
japo hatufahamu chanzo lakini pia bado hatujapata barua rasmi ya kuacha kazi
kutoka kwake,” alisema Mwesigwa.
Habari za ndani kutoka bodi hiyo, zimedai kuwa
tayari Mwakibinga amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kelele zinazoendelea kati
ya TFF na klabu.
0 COMMENTS:
Post a Comment