Juhudi za uongozi wa Simba kusaka kiungo mwenye
aina ya uchezaji kama kiungo wake wa zamani, Patrick Mafisango, zimeanza.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba
zimeeleza, kamati ya usajili imekuwa ikifanya juhudi kupata kiungo mchezeshaji
anayetembea na mpira na kutoa pasi za uhakika kama ilivyokuwa kwa marehemu
Mafisango.
Wakati wa Mafisango, Simba ilikuwa moto wa
kuotea mbali na ndiye aliendesha kikosi chenye historia ya kuitwanga Yanga kwa
mabao 5-0.
“Kweli juhudi zinafanyika, lengo ni kuwa na
kiungo wa aina ya Mafisango, kiungo anayetembea na mpira,” kilieleza chanzo.
“Hiyo ni kazi ya kamati ya usajili, tayari
imeanza kufanya kazi kwa kuwa upungufu mwingine unaonekana kuwa ni uchezeshaji.
“Kumekuwa na mawasiliano katika nchi mbalimbali
kuangalia aina ya kiungo kama Mafisango ili kuifanya Simba kuchangamka kwenye
kiungo.”
Mafisango alifariki kwa ajali ya gari ikiwa ni
siku chache baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba kuhusiana na suala
la kuongeza mkataba.
Simba imekuwa
ikihaha kuboresha kikosi baada ya kutoka sare sita mfululizo katika mechi zake
sita za ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment