Tukio la kumgonga dereva wa bodaboda
lililomhusisha beki wa Azam FC na Taifa Stars, Erasto Nyoni hatimaye
limemalizika salama.
Nyoni alitajwa kuhusika katika tukio hilo
lililotokea maeneo ya Manzese, Tip Top jijini Dar es Salaam na kuamua kukimbia
kisha kukamatwa akiwa maeneo ya Kijitonyama ambapo inadaiwa madereva bodaboda
walimshambulia kwa kumpiga.
Meneja wa Azam FC, Jemedari Said ameliambia
gazeti hili kuwa suala hilo limemalizika baada ya kushughulikiwa na viongozi wa
Azam FC.
Jemedari alisema hakuna dereva bodaboda
aliyejitokeza kudai kugongwa na Nyoni, hivyo wamelazimika kulipia gharama
mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo matengenezo ya gari aina ya Toyota Noah
linalomikiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd ambalo Nyoni aliligonga wakati
akiwa kasi.
“Kesho (leo) asubuhi anatarajiwa kuanza mazoezi
ya pamoja na wenzake baada ya tukio hilo kumalizika kwa ajili ya kuitumikia
timu yake,” alisema Jemedari.
Kwa upande wa Nyoni alisema: “Kikubwa
ninashukuru suala hilo limemalizika salama, kesho natarajia kuanza mazoezi na
wenzangu kwa ajili ya mechi ijayo.
“Ujue katika maisha misukosuko lazima itokee na
huwezi kujua leo Mungu anapanga nini, tukio hilo limetokea na limekwisha salama
nashukuru katika hilo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment