Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita,
Amissi Tambwe, ametua ofisini kwa Rais wa Simba, Evans Aveva na kukaa kwa zaidi
ya saa moja.
Tambwe, raia wa Burundi, alitua ofisini kwa
Aveva katika eneo la Posta jijini Dar es Salaam na kukaa ndani wakizungumza kwa
zaidi ya saa moja.
Baadaye ilielezwa, Tambwe na Aveva walikutana
baada ya mwaliko wa rais huyo aliyemwambia Mrundi huyo afike kwa ajili ya
mazungumzo.
Juhudi za kutaka kujua nini kilizungumzwa
zilikuwa na ugumu kwa kuwa Tambwe alikataa kuzungumza chochote wakati Aveva
hakupokea simu ya mkononi.
Taarifa za ndani zinaeleza kwamba, Aveva
alizungumza na Tambwe na kumueleza Simba haina mpango wa kumuacha kama ambavyo
imekuwa ikielezwa.
“Hata hivyo, rais alimtaka Tambwe kuongeza
juhudi, pia kuusikiliza uongozi badala ya zile taarifa ambazo amekuwa
akizisikia kupitia kwa mashabiki, wanachama au vyombo vya habari.
“Hivyo, amemtaka ajitume kwa ajili ya kuisaidia
Simba kwa kuelekeza nguvu zake kwenye timu badala ya kuingia hofu,” kilieleza
chanzo.
Tambwe amefunga bao moja tu hadi sasa, alikuwa
katika hofu kubwa kutokana na taarifa kama ataachwa kutokana kukosa nafasi ya
kutosha uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment