IVO |
Kipa wa Simba, Ivo Mapunda amewasili mjini
Tukuyu kwa ajili ya maandalizi ya mazishi ya mama yake mzazi.
Ivo amefiwa na mama yake ikiwa ni siku chache
baada ya kifo cha baba yake mzazi, Phillip Mapunda Februari, mwaka huu.
Awali Ivo aliiambia SALEHJEMBE kwamba yuko
njiani akisafiri kwenda Tukuyu kwa ajili ya mazishi.
Blogu hii inatoa pole kwa msiba huo kwa Ivo
pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment