November 26, 2014


Kiungo Emerson De Oliveira Roque amewasili leo akitokea kwao Brazil na kupokelewa na idadi chache ya mashabiki wa Yanga.

Imeelezwa Emerson ataanza majaribio kesho ingawa dalili zinaonyesha anaanza kazi moja kwa moja na Yanga.

Akionekana mwenye furaha, Emerson aliwapa mikono mashabiki kadhaa, baadaye akaongozana na Kocha Marcio Maximo na kiungo Coutinho hadi kwenye maegesho.

Emerson alipanda Hiace ya Yanga wakati Maximo aliondoka na msaidizi wake, Lonaldo Leiva.

Soma sifa za Emerson anayefananishwa na Yaya Toure wa Man City.

Kiungo huyo, ana sifa saba zinazofanana na za Yaya Toure ambazo ni kumiliki mpira, kupiga pasi fupi, kupiga pasi ndefu, kuokoa mipira kwa kulala ‘takolin’ na uwezo mkubwa wa kuokoa kwa kupiga vichwa, usisahau pia ni mzuri kwa mabao kwa kichwa.

Pasi:
Hapa ana sifa mbili, moja ni kupiga pasi fupi na ndefu za chinichini kwa uhakika kama ambavyo umekuwa ukimuona Yaya Toure.

Ukiangalia video hiyo ya ‘action zake’, utaona anavyotelezesha mipira, kwa pasi za chini za karibu na mbali. Sifa ya pili, anapiga zile pasi ndefu za juu na kweli zinafika.

Takolin:
Hapa ndiyo utampenda, ukiweka mguu, yeye anaweka mguu na nguvu alizonazo amekuwa akiiwahi mipira kwa kulala, anaokoa.

Nguvu:
Emerson ana nguvu za miguu, hivyo kumfanya awe bora katika ukabaji, iwe isiwe, Mbuyu Twite atalazimika kumpisha kwenye nafasi hiyo.

Vichwa:
Ukiangalia video hiyo, utaona ndiyo mchezaji anayepiga vichwa vingi vya kuokoa kwenye timu yake. Hivyo mipira mingi inayokwenda langoni mwake anaitoa.

Mabao:
Ndiyo, Emerson anafunga mabao hasa kwenye mipira ya adhabu inayochongwa langoni au kona. Uwezo wake ni kufunga kwa kichwa na amekuwa akifanya hivyo.

Mipira ‘iliyokufa’:
Maximo atalazimika kumpa nafasi, ili agawane na Coutinho namna ya kupiga mipira ya adhabu ndogo maarufu kama ‘mipira iliyokufa’. Ana uwezo wa kufunga kama ambavyo umekuwa ukimuona Yaya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic