MAXIME (MBELE)... |
Baada ya hivi karibuni kuibuka kwa tetesi kuwa
uongozi wa Simba una mpango wa kutaka kuwasajili mabeki wawili wa Mtibwa Sugar,
Salum Mbonde na Ramadhan Kessy, uongozi wa timu hiyo umekuja juu na kuionya
Simba kuachana na mpango huo.
Simba ina mpango wa kutaka kuwasajili nyota
hao ili iweze kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo inaonekana kutokuwa imara
kama kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, Patrick Phiri anavyotaka.
Kocha Mkuu
wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amedai kuwa ubora wa kikosi chake kwa sasa
unatokana na wachezaji hao ambao wanashirikiana vema na wengine, hivyo
haitakuwa rahisi kuwaachia katika kipindi hiki ambacho wanapigana kuhakikisha
msimu huu wanaibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara.
Alisema kama Simba inawahitaji, isubiri mpaka mikataba
yao itakapokuwa imemalizika ndiyo ianze mpango huo lakini kwa sasa itakuwa
vigumu kuwaachia.
“Mtibwa huwa hatuna tabia ya kuzuia wachezaji
wasiondoke ila kwa sasa itakuwa ni vigumu kidogo kwa sababu bado tunahitaji
huduma yao.
“Kama Simba watawasubiria mpaka mikataba yao
itakapofikia tamati basi tutawaachia waondoke,” alisema Maxime.
Mmmh,tutaona.
ReplyDelete