November 12, 2014

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’, amejikuta akiwachimba mkwara waandishi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutompiga picha alipokuwa akishuka kwenye gari lake kusikiliza kesi inayomkabili.


Tukio hilo lilijiri jana Jumanne ambapo Chid Benz alikuwa akikwepa kupigwa picha za wanahabari na kutoa baadhi ya maneno ya kuonyesha kuwa hakutaka kabisa kuwaona waandishi wakimzonga.

“Jamani picha mlizokwisha kunipiga hazijawatosha tu, tangu nilipokamatwa mmekuwa mkinipiga picha hazijawatosha? Leo sitaki,’’ alifoka mkali huyo wa kuchana ambaye ni kiongozi wa Kundi la La-Familia.

Chid Benz alifika mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya aina ya heroine yenye uzito wa gram 0.85, yenye thamani ya Sh 38,638, bangi yenye thamani ya Sh 1,720 pamoja na vifaa vya utumiaji wa madawa hayo haramu.
Hata hivyo, hakimu Waliarwande Lema, akiwa na mawakili wawili wa serikali, Ofmed Mtenga na Leonard Challo,  alisema kuwa upande wa jamhuri bado haujakamilisha upelelezi wa kesi hiyo, hivyo anaiahirisha mpaka Desemba Mosi, mwaka huu.


Chid Benz alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa safarini kuelekea Mbeya na sasa yupo nje kwa dhamana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic