LISITI YA SH MILIONI MOJA YA MALIPO YA RUFAA YALIYOFANYIKA OKTOBA 21....WAKATI JUZI TFF ILISEMA HAIKUWA IMEPOKEA RUFAA. |
Upambe kitu kibaya sana!Kuna kiongozi mmoja wa TFF
ambaye amekuwa akijitahidi kuandika matusi na kashfa kila stori ya TFF
inapowekwa kwenye blog hii.
Jana niliweka Memorandum of Appel aliyoipeleka Dk Damas
Ndumbaro TFF na ikapokelewa na Boniface Wambura.
Ajabu mtu huyo ambaye amekuwa akiandika matusi kuonyesha
si mtu mwelevu, asiye na hoja na anaonyesha picha halisi ya alipo, akasema eti
hiyo si rufaa akisisitiza SALEHJEMBE ana upeo mdogo na hajui lolote.
HII NDIYO RUFAA YA DK NDUMBARO KWA TFF... |
Kidogo inashangaza, ingawa ni jambo jema maana inasaidia
kujua nanihii anaungwa mkono na watu wa aina gani.
NITAMSAIDIA kidogo; Memorandum of appeal ndiyo rufaa
yenyewe na utaona kuna sababu nne za kukata rufaa zimeorodheshwa.
Alichokuwa anakizungumzia mpambe huyo wa nanihii ni
intension to appeal au intension to appeal, unaweza kusema nia au lengo la
kukata rufaa.
Sasa sijui kama kweli anajua sana sheria amefundishwa na
nani.
Najua anapigania maslahi ya TFF kwa kuwa anapata nafasi
ya kula.
Simkatazi kuchangia, Saleh Ally hajawahi kukwamishwa na
maneno ya shombo.
Fikria, leo mwaka wa 15 naandika michezo, matusi au
maneno mangapi ya shombo nimekutana nayo, bado nasonga, bado nasema ukweli na
siogopi.
Mara nyingi watu wengi wenye upeo mdogo au mduchu kabisa
hukimbilia matusi palipo na hoja msingi.
MNIAMNI, watu kama hao ndiyo wananipa nguvu ya
kutosimama na kuendelea kuonyesha ujinga na upuuzi walio nao.
Siku itafika nitawataja majina kwa kuwa nalifanyia kazi
kitaalamu kabisa. (JUU PALE KUNA LISITI, SASA KAMA INTENSION TO APPEAL NAYO INALIPIWA, BASI NI HATARI!)
MWISHO na msisitizo kwa Watanzania wenzangu, tutetee
maslahi ya mpira wetu, si matumbo yetu, tutakuwa wabinafsi.
Hoja za Dk Ndumbaro, zijibiwe kwa hoja, kama amekosea,
basi akosolewe bila ya woga pia. Lakini mambo hovyo na kuyumba kwa TFF au ubabe
unaotaka kufanya na shirikisho hilo, usipewe nafasi. TFF si ya mtu, mkoa wala
kundi la wapambe fulani ambao wameteuliwa kuwa viongozi kwa kuwa tu walishiriki
kampeni au walimsaidia Malinzi na sasa upuuzi wao wanauonyesha kwa kuzungumza
matusi zaidi, kuliko hoja za msingi kwa kuwa uwezo hauwaruhusu kwenda mbali
kihoja. MATUSI NDIYO NGAO YAO, KAMWE HAYATAWASAIDIA. WATSHINDWA TU.
Narudia kuweka risiti kuonyesha kuwa kweli Dk Ndumbaro
aliwasilisha rufaa kwa wakati mwafaka, pia naweka tena Memorandum of appeal,
bwana mpambe, hiyo ndiyo rufaa ndugu yangu, hakuna rufaa nyingine. Hehehe…
Kamwe usiwadharau watu kama hao kwani wengi wao wanataka kuelewa kupitia mabishano.
ReplyDeleteHongera Saleh kwa kuwaelewesha na kuwafanya wajue hiyo ni taaluma!