Kikosi cha Mwadui FC kimeendelea kupaa kwenye Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya kuichaoa Green Worriers kwa mabao 2-1, leo.
Kikosi hicho kinachonolewa na Jamhuri Kiwhelo 'Julio' kimeanza kushinda mfululizo zaidi ya mechi ya tatu baada ya kuanza ligi hiyo kwa kusuasua.
Upande mwingine, baada ya kuchapwa bao 1-0 na Lipuli ya Iringa katika mechi iliyopita, Villa ya Magomeni imebuka na kuilamba African Lyon kwa mabao 2-1.
Villa imeibuka na kuendelea kuididimiza Lyon huku ikionyesha soka safi.
0 COMMENTS:
Post a Comment