Kikosi cha JKT Ruvu kimeitwanga Ndanda FC kwa mabao 2-0.
JKT inayonolewa na Fred Felix Minziro imeshinda mabao hayo katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar.
Mabao ya JKT katika mechi hiyo yalifungwa na Najim Magulu kabla ya Samwel Kamutu kufunga bao la pili baada ya Magulu kupiga shuti kali na kipa kuutemba.
Ndanda imepokea kipigo kingine ikiwa ni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC ikiwa kwao Nangwanda Sijaona, Mtwara.
0 COMMENTS:
Post a Comment