November 21, 2014


Kesi ya aliyekuwa beki wa Simba, Mkenya, Donald Musoti dhidi ya timu yake ya zamani imesogezwa mbele na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) mpaka Februari, mwakani.


Simba iliondoa jina la beki huyo katika hatua za mwishoni kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwanzoni mwa msimu huu na kisha ikamsajili Emmanuel Okwi, raia wa Uganda.

Akizungumza na kutoka Kenya, Musoti alisema hukumu ya kesi yake dhidi ya Simba imesogezwa mpaka Februari, mwakani kutokana na kuwa wana kesi nyingi kwa sasa.

“Fifa wameamua kusogeza mbele hukumu ya kesi yangu dhidi ya Simba mpaka Februari, mwakani.

“Hata mwanasheria wangu Felix Majani ana imani ya kuwa nitashinda kesi kwa sababu ushahidi wa Simba ulitupiliwa mbali kutokana na kuchelewa kuutuma,” alisema Musoti.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic