Kiungo nyota wa Simba, Mganda,
Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa yupo Uganda katika mapumziko mafupi baada ya
kusimama kwa ligi, leo Jumatatu anatarajia kuanza rasmi matibabu ya maumivu ya
kifundo cha mguu wake wa kulia yaliyokuwa yanayomsumbua tangu kuanza kwa ligi
kuu msimu huu.
Okwi amesema iwapo atapona kabisa, basi anaamini makali yake yataongezeka maradufu.
Tayari amefumania
nyavu mara tatu katika mechi saba, alisema ndoto zake msimu huu ni kuhakikisha
Simba inafanya vizuri na kumaliza ikiwa na ubingwa wa ligi kuu (VPL), hivyo
anamwomba Mungu amjalie aweze kupona mapema jeraha hilo ambalo anasema
linamkosesha amani kila siku.
“Kesho (leo) ndiyo natarajia kuanza
matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu zote, hivyo namuomba Mungu anijalie
nipone mapema.
“Natamani safari hii kuiona Simba
inakuwa bingwa, hivyo ndoto hizo ili ziweze kutimia, inatakiwa wachezaji wote
kuwa fiti. Hivyo nawaomba wapenzi na mashabiki wa timu yetu waniombee ili
niweze kupona haraka,” alisema Okwi.
Uongozi wa Simba umepanga Okwi
kutibiwa na daktari maalum hukohuko kwao Uganda katika kipindi hiki ambapo ligi
imesimama.
0 COMMENTS:
Post a Comment