November 10, 2014


 Pichani shoto ni Mmoja wa Waimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Africans Star a.k.a Twanga Pepeta,Msafiri Diof  akiwa sambamba na skwadi zima la madansa wa bendi hiyo wakitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.


Wasanii wa music wa dansi Twanga pepeta na kikundi maarufu cha Tanzania House of Talent-THT jana walitikisa wakazi wa Dodoma katika viwanja maarufu vya vya Nyerere Squire kwa kutoa burudani kabambe wakati wa tamasha maalum la kuzindua huduma maalum ya Airtel ijulikanayo kama Airtel Money Timiza.

hafla hiyo ya uzinduzi wa mpya ya AIRTEL MONEY TIMIZA iliongozwa na MC maarufu nchini na mtangazaji wa redio bw, Taji Liundi ambapo alianza kwa kuikaribisha bendi ya Twanga pepeta na wasanii wa THT kupanda jukwaani kuomba umati wa wakazi uliofurika viwanjani hapo pamoja na wageni waalikwa kusimama na kukaa kimya kwa dakika chache ikiwa ni ishara ya kumkumbuka mwanamuziki mkongwe wa bendi hiyo Amigolas aliefariki Dunia mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam
Bendi nzima ya Twanga pepeta wakiongozwa na mwanamuziki mkongwe wa kundi hilo Luiza Mbutu pamoja na wasanii wengine kama msafiri diof, Buludoza, Saleh Kupaza na wengine wengi walishangiliwa sana na mamia ya waliohudhuria walipoimba nyimbo zao kama Mama vanesa, Aminata, Dunia daraja, Mwenda pole na kumalizia na burudani kali ya sebene walolocheza wageni waalikwa wote.
Baada ya twanga pepe na kufungua pazia kwa burudani hiyo  hafla ya uzinduzi wa Airtel money timiza ilizidi kunogeshwa na wasanii wa kundi maarufu nchini kutoka nyumba ya vipaji THT waliopanda jukwaani na staili maalum ya uchezaji kwajili ya uzinduzi wa huduma hiyo ya Airtel Money Timiza.
Nae mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso aliipongeza burudani zote na kuitambulisha huduma hiyo kwa mara ya kwanza akidai huduma ya Airtel Money Timiza ina lengo la kumsaidia mtanzania wa kawaida, makundi mbalimbali yenye uhitaji wa mikopo ya haraka na papo hapo bila kukumbana na mashari au kuweka amana ili apatiwe mkopo alima “Airtel Money ni mikopo ya kipekee nchini Tanzania ambapo mtanzania yeyote anaetumia huduma ya Airtel money anaweza kukopa kiwango anachohitaji mahali popote wakati wowote kwa kupiga tu *150*60# na kuchagua timiza”
Kwa upande wake Waziri wa mawasiliano sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawaaliizindua huduma hiyo kwa niaba ya Waziri mkuu Mh Mizengo Pinda akiipongeza Airtel kwa kuunga mkono serikali yake kwa kusema “Airtel hii taarifa ya mikopo ya TIMIZA ifikisheni katika maeneo yote hasa vijijini ambako bado huduma za benki na mikopo ni ngumu kupatikana”
Kampuni ya Airtel imejipanga kufanya utambulisho wa huduma ya Airtel Money Timiza katika mikoa yote kwa lengo la kuongezea wananchi ufahamu juu ya Mikopo hiyo nafuu na rahisi na  hatimae kuongeza fulsa kwa wajasiliamali  katika shughuli zao za uzalishaji


Mmoja wa Waimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Africans Star a.k.a Twanga Pepeta,Msafiri Diof  akitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Pichani shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi akijimwaya mwaya jukwaani wakati wa uzinduzi rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.pichani kati ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.


Baadhi ya Wasanii kutoka nyumba ya vipaji THT,wakitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Squea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic