Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
iliyokutana jana (Desemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, imezingatia
upungufu uliopo katika utekelezaji wa matumizi ya tiketi za elektroniki.
Hivyo, Kamati hiyo imeiagiza Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na
benki ya CRDB inayoendesha mfumo huo wa matumizi ya tiketi za elektroniki
kuhusu upungufu huo na kuhakikisha unafanyiwa kazi.
Tiketi hizo zimeonekana
kutokuwa na mafanikio wakati wa majaribio yake.
Katika viwanja kadhaa
ikiwemo Mkwakwani mjini Tanga, watu walishindwa kuingia uwanjani baada ya
mashine za ukaguzi wa tiketi kuharibika.
Hali hiyo ilisababisha
mashabiki waliokuwa wamejazana kwa wingi kuvunja geti na kuingia ndani.
Pia zimeonekana zimekuwa
hazina ulinzi wa kutosha kwani kuna baadhi ya mashabiki wa Simba walikamatwa na
tiketi za wizi ambazo zilikuwa ni sahihi kabisa na zile zinaztumika.
Mashabiki hao walikamatwa
katika mechi kati ya Simba dhidi Mtibwa Sugar iliyokuwa inapigwa kwenye Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment