Sasa si hadithi tena,
hatimaye mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki amesaini mkataba wa
mwaka mmoja kuichezea Ruvu Shooting.
Mwombeki ambaye aliachwa na
Simba na baadaye kwenda Oman kufanya majaribio ambako imeelezwa hakufuzu,
amesaini kuichezea Ruvu Shooting leo.
Maana yake, mshambuliaji
huyo ataanza kuonekana kwenye mechi za Ligi Kuu Bara zitakazoanza tena Desemba
26, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment