Mrundi, Amissi Tambwe, aliyejiunga na Yanga, ametokwa na udenda huku akishangaa namba mchezaji mwenzake Mbuyu Twite anavyoishi raha mustarehe tofauti na yeye alivyokuwa akiishi wakati akiwa Simba.
Tambwe alimtembelea Twite nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, na kujikuta akijiuliza namna alivyokuwa akiishi katika nyumba aliyopangiwa Simba kama ilikuwa sahihi.
Tambwe alikumbwa na hali
hiyo bila ya kutegemea kutokana na kujionea maisha mazuri ambayo anaishi beki
huyo huku akiambiwa kuwa na wachezaji wengine wa timu hiyo nao wanaishi vizuri
kama ‘professional’.
Tambwe amesema hali hiyo imefanya Tambwe ajione kama mtu
aliyekuwa amepotea lakini mwisho wa siku anaamini kuwa hivi sasa naye ataishi
maisha mazuri kama wachezaji wenzake wa kimataifa wa Yanga.
“Maisha aliyokuwa akiishi
Simba siyo kama ya mchezaji wa kulipwa, yalikuwa ya kawaida sana ila kwa sasa
kutokana na utamaduni wa Yanga wa kuwajali wachezaji wake ataishi kwa amani na
atafanya kazi yake kwa moyo mmoja.
“Alipokuwa Simba alikuwa
akiishi kama yupo jeshini, nyumba moja watu kibao ukikaa vibaya vitu vyako
unaibiwa lakini sasa anaamini ataishi kwa amani kabisa,” alisema mtoa habari
huyo na kuongeza:
“Watu wengi najua hawataamini juu ya hili lakini ukweli ndiyo
huo, Yanga inawajali sana wachezaji wake ukilinganisha na Simba na kama
hawaamini basi watembelee sehemu ambazo wachezaji hao wanaishi na watapata
jibu.”
Tambwe amejiunga na Yanga
kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao utamwezesha kujikusanyia jumla ya Sh milioni
78. Milioni 34 zinatokana na usajili wake na zilizobakia zinatokana na mshahara
wake atakaokuwa akilipwa kwa mwezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment