Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, ametoa yake ya moyoni
na kusema kuwa kama kweli Yanga imemtimua kocha wake, Mbrazili, Marcio Maximo
basi haikuwa sahihi kwa sababu alikuwa tayari ameshakaa katika mstari.
Kocha huyo aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Zambia 'Chipolopolo',
amesema kuwa, kitendo cha klabu kutimua makocha baada ya
muda mfupi si kizuri kwa sababu kinaharibu programu za mwalimu husika, ingawa
hawezi kuingilia masuala ya Yanga.
“Unajua kila kocha ana vitu vyake anavyovifanya katika timu, sasa
ikitokea akatimuliwa kabla hajakamilisha ni tatizo, kwa kuwa atakayekuja
ataanza upya.
“Uongozi wa Yanga una kitu umeona unataka kurekebisha na njia
mojawapo ni kutokuwa na Maximo, hilo siwezi kuwashambulia kwa sababu wao wanaijua
zaidi Yanga.
“Nilikutana naye (Maximo) na tulizungumza baada ya mchezo, Maximo ni
rafiki yangu mkubwa tunapokutana nje ya uwanja, ninafikiri huu ni muda mzuri wa
kujitafakari, makocha kufukuzwa ni kawaida, ninafikiri analijua hilo,” alisema
Phiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment