December 19, 2014


Licha ya Simba kumtoa kwa mkopo kiungo wake, Haruna Chanongo kwenda Stand United, mchezaji huyo amepokewa kwa mikono miwili na mashabiki wa Mkoa wa Shinyanga.


Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu, amesema kuwa mashabiki wamefurahishwa na ujio wa Chanongo katika timu yao, ndiyo maana walimpokea kwa shangwe nyingi kwa kuwa wanajua ni mchezaji mzuri.

“Mashabiki wa Stand kiukweli wamefurahia ujio wa Chanongo na wamekuwa wakitembea na mabango na kuimba kuwa wana imani na kiungo huyo.


“Anatarajiwa kuanza mazoezi kesho (leo) Ijumaa jioni au kesho baada ya kupumzika na uchovu, aliingia yeye pamoja na Peter Mutabuzi, nahodha msaidizi na Abuu Ubwa,” alisema Kanu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic