December 21, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amewataka wachezaji wake kutoamini ushindi wa mchezo mmoja, badala yake kujiandaa upya kila baada ya mechi moja.


Phiri amesema kikosi chake kinaanza kuonyesha mabadiliko tofauti na ilivyokuwa awali, lakini suala la kujituma halikwepeki.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Phiri amesema kila baada ya mechi moja ni maandalizi ya mechi nyingine.

"Ukishinda moja, unaanza kuwaza nyingine. Ushindi mmoja haukamilishi kila kitu au sare au kupoteza mara moja, hakupotezi kila kitu.

"Nazungumza sana na wachezaji pamoja na wasaidizi wangu, wanajua haya ninayokuambia.

"Simba ni timu kubwa sana na kila mmoja angefurahi kuiharibia, kila anayejua anakutana na Simba, maandalizi yake yanapanda maradufu.

"Sasa kwa mchezaji aliye Simba, maandalizi yake yanatakiwa kuwa maradufu kila siku kwa kuwa kila mechi ni dhidi ya walioajiandaa maradufu," alisema Phiri.

Tayari Simba iko kambini Zanzibar kujiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic