Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa.
Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.
"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.
"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.
Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.
"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.
Sidhani kama haya ni maamuzi sahihi, kuna watu ambao mmekuwa karibu kabisa na simba nikimaanisha viongozi na wachezaji pamoja na kuujua vizuri mfumo wa uongozi wa club ya simba, kikubwa nilichokiona kupitia makala zenu mbalimbali kinachoonekana tatizo simba sio kocha, kuna mambo mengi yanayosababisha mambo yawe hivi, tunazidi kufanya makosa kila kukicha kwa nn viongozi wasitulie katika kufanya maamuzi, hivi ni kweli huwa wanakaa na kuchambua nn chanzo cha tatizo au ndo kama inavyoaminika ni matakwa ya wachache wenye sauti, huu ni ujinga, mashabiki tunaumia sana na ni kwa sababu tu tumeanza kuipenda Simba tungali tukiwa wadogo sana kwa hiyo kuihama ni ngumu. Na tatizo kubwa la mpira wa tz viongozi wa soka ni walewale kuanzia kwenye ngazi ya juu yaani TFF hadi kwenye hzclub zetu, hakuna mawazo mapya tunaendesha mpira ule ule wa miaka mingi iliyopita, kiukweli hatutaendelea kamwe na Simba matatizo hayatokwisha kwa style hii...Bado nina imani na kocha Phiri, angeweza kutufikisha sehemu flani nzuri kama hayo matatizo mengine yangepatiwa ufumbuzi..
ReplyDeletecoaches are hired to be fired bro, huu ndo mpira.
Deletesimba haifanyi vizuri hakuna tatizo zaidi ya kocha, nje ya hapo utakuwa sio mtu wa football but unaye amini mpira unachezwa nje ya uwanja, kosa pekee walilolifanya viongozi wa Simba ni kuchelewa kugundua kuwa kuna tatizo katika benchi la ufundi, matokeo yake wakaingia katika siasa za Mpira Pesa na Ukawa!! makocha huwa wanafikia pahali wanakuwa hawana jipya tena katika club achilia mbali uwezo mkubwa walio nao, thats why coaches like Morinho wanahama vilabu kila kukicha, da same to Benitez, Anchelot n.k sio kwamba hawana uwezo la hasha ispokuwa wanakuwa hawana jipya tena katika club husika.
so i belive this is right decision though imekuja late sana.