Kikosi cha Simba kimefanikiwa kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vijana.
Mechi hiyo kati ya Simba A dhidi ya Simba B
imepigwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo.
‘Aliyewaua’ vijana hao ni mshambuliaji Elius
Maguri lakini kiungo Omar Mboob raia wa Gambia akawa kivutio.
Mboob alionyesha kuwavutia mashabiki
waliojitokeza alipoingia mara ya pili.
Alicheza mara ya kwanza, lakini hakuonekana
kuchangamka sana hadi alipoingia katika kipindi cha pili na kufanya vizuri.
Mgambia huyo yuko katika majaribio ya
kuichezea Simba.
Nimpongeze Maguri kwa alichokifanya katika game ya leo! Lakini changamoto iliyo mbele yake ni kubwa na anatakiwa kujipanga zaidi! Naamini Maguli ndiye mshambuliaji bora kwa sasa katika washambuliaji wa ndani, so ujio wa mastriker wa nje umfanye
ReplyDeletekuonesha thamani yake na si kukata tamaa! akiamua anaweza!