![]() |
| COUTINHO... |
Bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Han van Der Pluijm,
amembadilishia jina kiungo wake mshambuliaji, Andrey Coutinho na sasa anamuita
Romario de Souza Faria.
Romario ni straika wa zamani wa Brazil
aliyetamba miaka ya 1990 mpaka 2000, hasa kwenye kikosi cha taifa cha Brazil.
| PLUIJM |
Kocha huyo raia wa Uholanzi, alianza kusikika
akimfananisha Coutinho na Mbrazili mwenzake huyo katika mazoezi ya Yanga
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio jijini Dar es
Salaam, juzi.
Pluijm alikuwa akimuita Coutinho kwa jina hilo
la Romario kila alipokuwa akitaka kutoa maelekezo kwake na kiungo huyo hakusita
kuitikia.
Alipoulizwa kocha huyo sababu ya kumuita jina
la Romario alifunguka: “Sitamuita jina la Coutinho tena, sasa nitamuita Romario
kutokana na aina yake ya uchezaji kufanana na Romario.”








0 COMMENTS:
Post a Comment