| MWALALA WAKATI AKIICHEZEA YANGA... |
Katika hali ya sintofahamu, Kocha Msaidizi wa
Coastal Union, Ben Mwalala, ametimka katika kikosi hicho na kurejea nchini kwao
kutokana na kuwepo kwa madai ya masuala ya kimaslahi na nafasi yake kuchukuliwa
na aliyekuwa kocha wa Mgambo msimu uliopita, Mohamed Kampira.
Mwalala alikuwa akisaidiana na Mkenya mwenzie,
Yusuf Chipo ambaye naye alibwaga manyanga katika kikosi hicho kwa madai
anakabiliwa na matatizo ya kifamilia na kushindwa kurejea nchini.
“Mwalala ameondoka kutokana na masuala ya
kimaslahi baada ya kushindwana na klabu, japo mpaka sasa haijaweka wazi suala
hilo na hii inakuwa kama ilivyotokea kwa Chipo,” kilisema chanzo.
Ofisa Habari wa Coastal, Oscar Assenga
ambaye amesema: “Mwalala hayupo na sina taarifa zozote, kuhusu Kampira
kuonekana kwenye benchi siyo tatizo, ni mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi
la timu yetu.”







0 COMMENTS:
Post a Comment