Kocha Mkuu wa Yanga, Hans
van der Pluijm amemuweka faragha kiungo wake Andrey Coutinho raia wa Brazil na
kufanya naye mazungumza.
Habari za uhakika kutoka
Yanga zimeeleza kwamba Pluijm raia wa Uholanzi alikaa na Coutinho na kuzungumza
naye mambo kadhaa kuhusiana na timu.
“Kweli kocha alikaa na
Coutinho tukiwa Zanzibar na kumtaka acheze soka, ajiamini na ajue kazini pia
aachane na maneno ya hisia.
“Unajua awali kulikuwa na
taarifa kwa kuwa Mbrazili mwenzake, Marcio Maximo ameondoka basi Pluijm
hatampanga,” kilieleza chanzo.
Baadaye juhudi za kumpata
Pluijm kuhusiana na suala hilo zilifanikiwa, naye akasema kuzungumza na
mchezaji wake ni jambo la kawaida.
“Ninazungumza na Coutinho
na wachezaji wengine mara kadhaa. Maneno yanaweza kuwa ya aina nyingi, lakini
najua Coutinho ni mchezaji anaijua kazi yake.
“Pia niseme, Coutinho ni
mchezaji mzuri. Hivyo ninaweza kumhimiza ajitume au kubadilisha kitu na kukaa
naye si jambo geni,” alisema Pluijm.
Maximo alitupiwa virago
vyake na nafasi ikachukuliwa na Pluijm ambaye anaonekana kuibadili timu na sasa
inacheza kwa kasi kubwa.








0 COMMENTS:
Post a Comment