Kocha wa Simba, Goran
Kopunovic ametangaza mapemaa kwamba aina tatu za wachezaji hawawezi kudumu
katika kikosi chake.
Kopunovic raia wa Serbia
amesema wachezaji wasiotaka kujituma ndiyo kundi la kwanza hawatakuwa na nafasi
katika kikosi chake.
“Pili ni wale wasiokuwa
na nidhamu na tatu wasiocheza kwa manufaa ya timu au kuangalia manufaa ya
pamoja kama timu, hakika hawawezi kukaa na mimi,” alisema Kopunovic.
“Mimi naamini katika
kukosea, lakini nisingependa kuona mtu asiye na nidhamu au asiyejituma au
mbinafsi anaangalia maslahi yake, hawezi kuwa na nafasi kabisa.”
Kopunovic alisema kwa
kuwa anaamini katika kukosea kwamba binadamu anapokesea na kurekebisha makosa
yake anakuwa bora zaidi, basi yuko tayari kuvumilia mambo mengi.
“Si lahisi kwa kosa moja
ukaamini mtu ana matatizo, wote tunakosea lakini anayerudia kukosea kila mara
anakuwa si mtu mzuri,” alisisitiza.
Kocha huyo atakuwa na
mtihani wake wa kwanza wa ukweli wakati atakapoingoza Simba katika mechi yake
ya kwanza ya Ligi Kuu Bara.
Simba itakuwa inacheza
mechi yake ya tisa ikiwa ugenini dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara lakini itakuwa
ni mechi ya kwanza ya Mserbia huyo.
Kabla ya hapo, Simba
imecheza mechi nane chini ya Mzambia Patrick Phiri, ikashinda moja, sare sita
na kupoteza moja.








0 COMMENTS:
Post a Comment