January 21, 2015


Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amewataka wapenda soka nchini kutoingiza ushabiki katika suala lake la kukabwa shingoni na beki wa Ruvu Shooting, George Michael.


Tambwe amesema anaumia sana kutokana na maneno makali au alivyodhalilishwa na mabeki wa Ruvu Shooting hivyo lisingekuwa jambo jema watu kuingiza ushabiki wa Yanga na Simba.

"Najua kuna ushindani mkubwa wa Yanga na Simba, lakini hili si suala la ushabiki ni kwa ajili ya maendeleo ya soka ya Tanzania.

"Lazima kuwe na wageni ili mpira uendelee. Hata Burundi hawalipi fedha nyingi lakini kuna wageni wako pale.

"Kama watu watakuwa wanadhalilishwa, wanatupiwa maneno mabaya kama ya kukumbushiwa vita, kuitwa wakimbizi, ni kuurudisha nyuma mpira.

"Suala hili naliachia uongozi wa Yanga pia TFF ambao naamini wanatakiwa kuchukua hatua kwa sheria zao," alisema Tambwe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic