Uongozi
wa CSKA Moscow kupitia mtandao wake umesema bado hauna uhakika kuhusiana na
suala la Mbwana Samatta.
Mtandao
huo umesema ni mapema kuzungumzia suala la Mtanzania huyo ambaye yuko katika
timu hiyo anafanya majaribio.
CSKA
imemchukua Samatta ambaye anendelea na mazoezi akiwa na timu nchini Hispania.
“Bado
ni mapema, huenda tusimchukue lakini benchi la ufundi lina nafasi ya kuendelea
kumuangalia,” ilisema sehemu ya mtandao huo.
Samatta
anayekipiga TP Mazembe anawaniwa na zaidi ya timu nne za Ulaya ambazo ziko
tayari afanye majaribio.
0 COMMENTS:
Post a Comment