| MWAMUZI WA AKIBA AKITIMUA MBIO HUKU MMOJA WA VIONGOZI WA POLISI TABORA AKITAKA KUMKAMATA... |
Waamuzi wengine wamepigwa
tena na timu inayomilikiwa na Jeshi la Polisi Tanzania!
Mamuzi wa kati na msaidizi
wake wameambulia kipigo jana kutoka kwa wachezaji wa Polisi Tabora.
Kipigo hicho wamekipata
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ikiwa ni siku moja baada ya
wachezaji wa Polisi Dodoma kwenye uwanja huo kumtandika mwamuzi.
Wachezaji wa Polisi Tabora
waliingia jazba baada ya Toto African kusawazisha bao na kuongeza jingine ndani
ya dakika mbili tena dakika ya 90.
Baada ya bao la pili
walimvamia mwamuzi wa akiba Agustine Mapalala wa Geita maarufu kama mshika kibendera na kuanza kumshushia
kipigo.
Alipoona mambo magumu
alianza kutimua mbio na wao wakahamishia hasira zao kwa mwamuzi wa kati Jamada Amada kutoka Kagera.
Hata hivyo, askari
waliokuwa uwanjani waliamua kuingilia na kuzuia tukio hilo na mwamuzi
alikimbizwa kwenye chumba cha VIP.
Baadaye mwamuzi alirudi
chini ya ulinzi mkali na kumaliza mpira huku tayari wachezaji wa Polisi Tabora
wakiwa wametoka nje ya uwanja.







0 COMMENTS:
Post a Comment