Kocha Mkuu wa Yanga, Hans
van der Pluijm ameonyesha kutilia mkazo katika suala la kutengeneza nafasi na
kuzutumia.
Katika mazoezi ya leo
alitumia zaidi ya nusu saa akiwanoa wachezaji wake hasa walio kwenye safu ya
ushambuliaji kama Kpah Sherman, Coutinho, Mrisho Ngassa, Amissi Tambwe, Nizar
Khalfan, Jerry Tegete na Simon Msuva.
Pluijm alikuwa akiwanoa
washambuliaji wake hao kuhusiaa na suala la kutulia kila wanapotakiwa
kuutumbukiza mpira wavuni.
Mholanzi huyo amekuwa
akilalama kwamba wanapata nafasi, lakini hazitumiki.
“Ni kati ya mambo
niliyotilia mkazo. Tunahitaji mabao na ikiwezekana mengi na mechi ya wikiendi
hii itakuwa kipimo kwa tunachofanya sasa,” alisema Pluijm.







0 COMMENTS:
Post a Comment